This archive report was first published on 1 July 2020.
Hospitali ya Shalom, Athi River yafunguliwa tena ¶
Hospitali ya Shalom iliyoko Athi River ilifunguliwa tena baada ya wagonjwa wawili kuangamizwa na COVID-19.
Mkurugenzi wa KMPDC Daniel Yumbya alisema uamuzi huo unafuatia ripoti iliyotolewa Jumatatu kwa baraza hilo na Serikali ya Kaunti ya Machakos.
Yumbya aliagiza usimamizi wa hospitali hiyo kuhakikisha kuwa kituo hicho kinapulizwa dawa na usafi wa hali ya juu unafanyika.
Awali watu 16 wakiwemo wahudumu wa afya wa hospitali hiyo walithibitishwa kuambukizwa coronavirus.
Hospitali ya Shalom ilifungwa siku tatu zilizopita baada ya wagonjwa kufariki kufuatia COVID-19.
Gavana wa Machakos Alfred Mutua aliilaumu hospitali hiyo kwa kuwalaza wagonjwa wanne waliokuwa wakiugua COVID-19.
Aidha KMPDC iliagiza zaidi Mkurugenzi wa Afya katika Serikali ya Kaunti ya Machakos kuhakikisha wahudumu wa afya walioambukizwa COVID-19 wamewekwa katika karantini maalum katika hospitali hiyo.