This archive report was first published on 30 June 2020.
COVID-19: Spika wa Bunge la Kitaifa akiri Wabunge 2 wanaugua Virus ¶
Kufikia Jumanne, Juni 30, visa 176 vipya vya corona vilithibitishwa nchini Kenya na kufikisha idadi ya maambukizi jumla ya maradhi hayo kuwa 6,366.
Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi, amefichua kuwa wabunge wawili wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona. Wabunge hao wameambukizwa baada ya kupimwa kwa sampuli za virusi.
Wabunge hao wameambukizwa baada ya kupimwa kwa sampuli za virusi. Muturi anasema tayari mbunge mmoja ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kutopatwa na virusi hivyo na anajifanyia karantini ya binafsi nyumbani kwake huku mmoja akisalia hospitalini.
Spika huyo alipuzilia mbali ripoti ya awali kuwa wabunge sita wanaugua virusi vya corona. Picha: Daily Nation.
Wagonjwa wapya walioambukizwa walithibitishwa baada ya sampuli 2,419 kupimwa katika muda wa saa 24 zilizopita. Kulingana na Katibu Msimamizi wa Afya Rashid Aman wagonjwa wote ni Wakenya huku 100 wakiwa wanaume na 76 wanawake.