Skip to main content

Polisi wa Kirinyaga wamkamata mwanamume anayedaiwa kumwua mpenziwe na kumzika

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 30 June 2020.

Polisi wa Kirinyaga wamkamata mwanamume wa miaka 34 anayedaiwa kumwua mpenziwe na kumzika nyumbani kijijini cha Kianderi.

Naibu Kamishna wa Kirinyaga ya Kati Daniel Ndege aliiambia Tuko kwamba mshukiwa Simon Murimi Wanjohi alikamatwa Jumapili, Juni 28, mtaani Baricho, eneo bunge la Ndia saa tisa asubuhi.

Alisema mshukiwa alifumaniwa na babake akichimba shimo bomani mwake Jumanne, Juni 23, lakini alipomuuliza ni la kufanya nini alisema ni la kutupa taka.

Aliporejea nyumbani kwa mwanawe siku iliyofuata, alikuta shimo hilo limefunikwa na akawaarifu chifu na majirani waliolichimbua.

Waliona miguu ya mtu na ndiposa wakabaini kuwa jamaa alikuwa amezika mwili.

Mamake marehemu, Beatrice Kabari alisema mwanawe alitoweka Jumatatu.

Polisi walikuwa wameufukua mwili wa mwanamke huyo Ijumaa na kuupeleka katika hospitali ya Kerugoya ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →