Skip to main content

Arsenal yalima Sheffield United 2-1 kufuzu kuingia nusu fainali ya FA

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 28 June 2020.

Arsenal yalima Sheffield United 2-1 kufuzu kuingia nusu fainali ya FA

Ushindi wa Arsenal dhidi ya Sheffield United katika uchanjio wa Bramall Lane Jumapili, Juni 28, 2020, ulimfanya kufuzu kuingia nusu fainali ya Kombe la FA.

Magoli ya Nicolas Pepe na Dani Ceballos yalitosha Gunners kupata ushindi huo mkubwa huku ikisajili ushindi mfululizo kwa mara ya kwanza tangu kurejea kwa kabumbu.

Pepe alikaribia kufunga bao lake la pili baada ya kuchongewa krosi na Kieran Tierney na kupiga shuti akiwa mbali, awamu ya kwa kwanza ikitamatika 1-0 kwa faida ya Gunners.

Wakati wa kipindi cha pili, David Luiz ambaye alikuwa anawakilisha Gunners kwa mara ya kwanza tangia kutumikia marufuku ya mechi mbili, aliuguza jeraha la mguu na kutwaliwa na Rob Holding.

Sheffield United walipata bao la kusawazisha dakika ya 87 huku Chris Robinson akivurumisha kombora kali lililotua ndani ya sanduku, na mpira huo ulimwangukia vyema David McGoldrick na kuipoteza akiwa yadi nne.

Lakini Arsenal ndio walicheka na wavu mara ya mwisho huku mchezaji wa akiba Dani Ceballos kuchukua mpira telezi na kufunga karibu na lango katika dakika za kwanza za muda wa kuongeza na kubeba Arsenal kuingia nusu fainali.

Ndoto ya Arsenal ya kubeba taji lao la 14 la Kombe la FA bado ni imara kupitia bao hilo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →