Skip to main content

UN Yashtushwa na Video ya Ngono Nchini Israel

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 28 June 2020.

UN Yashtushwa na Video ya Ngono Nchini Israel

Umoja wa Mataifa umeshtushwa na video ya ngono iliyozagaa ndani ya gari lake nchini Israel.

Video iliyozagaa katika mitandao ya kijamii inaonyesha mwanamke akiwa amemkalia mwanamume katika kiti cha nyuma cha gari lenye nembo ya UN wakifanya madhambi.

Wale waliohusika wanaaminika kuwa maafisa wa kulinda amani nchini Israel na wanakaribia kutambuliwa.

Umoja wa Mataifa una sheria kali dhidi ya tabia za ngono miongoni mwa wafanyakazi wake na wanaweza kuadhibiwa iwapo watakiuka sheria hiyo.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukichunguzwa kufuatia madai ya dhuluma za ngono ambayo imekuwa ikiwahusisha maafisa wake na wasichana wachanga.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aliahidi kukabiliana na shutuma za utovu wa nidhamu wa kingono katika muungano huo.

Video iliyozagaa katika mitandao ya kijamii ilidaiwa kunaswa katika barabara kuu mjini Tel Aviv.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba umekerwa na kanda ya video ya ngono.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →