Skip to main content

Seneta mteule Isaac Mwaura asherehekea miaka mitano katika ndoa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 28 June 2020.

Seneta mteule Isaac Mwaura na mkewe wanasherehekea miaka mitano tangu walipofunga pingu za maisha.

Alisema anamshukuru Mungu kwa umbali amemtoa pamoja na familia yake.

Ingawa alielezea changamoto kadhaa ambazo wamekumbana nazo katika ndoa, seneta huyo alisema ndoa yao imenawiri.

Aliongeza kuwa ndoa imewafunza mambo mengi ikiwemo kufaana kwa lolote, kuheshimiana na kuwa waaminifu.

Alisema miaka mitano iliyopita, mimi na Mukamu Rwamba tulifunga pingu za maisha katika sherehe ya kufana katika uga wa Evergreen Park na kisha Ikulu.

Seneta huyo pia alikumbuka jinsi alifiwa na watoto lakini kwa yote anamshukuru Mungu kwa sababu amemjalia mtoto mmoja wa kiume.

Aliongeza, "Tumeshinda vita mingi, tumepigana na kugombana, tumekata tamaa, tumefiwa watoto lakini tunamshukuru Mungu ametujalia Njiru, kwa sasa tunaishi maisha kama ya watu wengine, tumeweka imani yetu na urafiki kwa pamoja," Aliongeza Mwaura.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →