This archive report was first published on 27 June 2020.
Gavana Mike Sonko alinunua bidhaa zote za akina mama wachuuzi Othaya na kuchangamsha kina mama hao baada ya kununua bidhaa zote.
Alinunua bidhaa kwa KSh 3,000 kwa kila kitu na kuwapa kina mama hao.
Wasaidizi wa Sonko walichukua bidhaa hizo na kuzitia kwenye magari yake kabla ya msafara wake kuondoka.
Msaidizi wa Sonko alisema wanaelekea nyumbani kwa rais mstaafu Mwai Kibaki.
Alisema, "Wacheni sasa tuende kuona mzee Kibaki," huku msafara huo ukiondoka.
Alitoa maski kwa wachuuzi ambao hawakuwa nazo huku akiwataka kuzingatia sheria ya kutokaribiana.