This archive report was first published on 27 June 2020.
Wakazi wa Lessos wakataa ujumbe wa Rais ¶
Wakazi wa Lessos, Nandi Hills, walikataa ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta alipokuwa akizungumza eneo hilo Ijumaa, Juni 27, 2020.
Alipokuwa akizungumza, Mbunge wa Nandi Hills Alfred Keter alisema kuwa amefika na ujumbe mzito wa viongozi wengine na maafisa wakuu wa polisi waliotumwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Alisema Rais Uhuru Kenyatta alifadhaishwa na kisa hicho na atahakikisha kuwa haki inafanyika kwa familia zilizoathirika.
"Sababu tuko hapa na maafisa wakuu wa usalama ni kwa sababu wametumwa na rais. Amefadhaishwa na kilichotokea kwa watu wa Lessos na ametuma rambirambi zake," alisema Keter.
Walakini, Keter alikatizwa na kuulizwa ametumwa na nani huku akitakiwa kutoa rambirambi za DP Ruto pekee.
Wakazi walimwambia Keter, "Tuambia kuhusu Ruto. Hatutaki kuskia hao wengine," huku wakikubali kuskiza ujumbe wa mbunge huyo ambaye ni mkosoaji wa DP.
Alfred Keter ni mmoja wa wabunge kutoka Bonde la Ufa ambao wanampinga DP Ruto na siasa zake za 2022.