This archive report was first published on 27 June 2020.
Maafisa wa polisi waliarifiwa na mmoja wa jamaa za mshukiwa kuwa alionekana akichimba kaburi ambalo baadaye alilifunika kwa mchanga.
Mwili wa mwanamke mwenye umri wa miaka 27 aliyezikwa katika kijiji cha Kianderi, eneo bunge la Kirinyaga ya Kati ulifukuliwa Ijumaa, Juni 26, 2020 na maafisa wa polisi.
Marehemu aliyetambulika kama Eunice Wambui anaaminika aliuawa na mpenziwe Simon Murimi mwenye umri wa miaka 35.
Maafisa wa polisi waliarifiwa na mmoja wa jamaa za mshukiwa kuwa alionekana akichimba kaburi ambalo baadaye alilifunika kwa mchanga.
Mwili wa mwendazake umelazwa katika makafani ya Kerugoya ukisubiri kufanyiwa upasuaji huku polisi wakimsaka mshukiwa.
Video ya Citizen Digital inaonyesha mshukiwa akichimba kaburi.