Skip to main content

Gavana Waiguru: Mumewe Ni 'Mume Kutoka Binguni'

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 27 June 2020.

Waiguru: Mumewe Ni 'Mume Kutoka Binguni'

Gavana Ann Waiguru wa Kirinyaga amemtunuku mumewe, Kamotho Waiganjo, sifa sifufu kwa kumtetea katika mashtaka yaliyokuwa yakimwandama katika Seneti.

Waiguru alisema hii wakati wa kujibu mashtaka yaliyokuwa yakimwandama katika Seneti, ambayo ilikuwa inahusisha mashtaka ya kupotea kwa pesa katika ofisi yake.

Waiguru alisema tofauti na akina mama wengine ambao wapenzi wao walikuja wakitembea, wake alitoka binguni.

"Natoa shukran za kipekee kwa mume wangu ambaye amekuwa akiniunga mkono kipindi hiki chote," alisema Waiguru.

Waiguru aliongeza, "Rafiki yangu hivi karibuni aliniambia kuwa kuwa wapenzi kutoka binguni na wale ambao hujileta. Kwa kweli wewe ulitoka juu binguni," alisema Waiguru.

Waiganjo aliongoza kikosi cha mawakili wa Waiguru katika kesi hiyo, na alijihami na kumtetea mpenziwe akipuuza ushahidi ulioleta na MCAs.

Alisema licha ya kuwa kulikuwa na madai kadhaa, hakuna hata moja ambalo lilikuwa limedhibitishwa kumhusisha Waiguru.

"Maseneta, angalau kunafaa kama kuna madai ya kupotea kwa pesa ionekana zilitolewa hapa na kuwekwa hapa na fulani ndiye alifaidika," alisema Waiganjo na kuitaka kamati ya seneti kutupilia mashtaka yote.

Waiganjo ni mumewe wa Waiguru, na wawili hao walioana mwezi Julai mwaka wa 2019 baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa muda.

Wawili hao walipeana talaka na wapenzi wao wa kwanza kabla ya kuingia kwenye uhusiano wao.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →