This archive report was first published on 26 June 2020.
Wanyama, ambaye anafanya kazi na Royal Media Services runinga ya Citizen TV, alipokea vitisho baada ya kufanya taarifa kuhusu maandamano ya wakazi wa Kesses waliokuwa wakilalamikia hali mbovu ya barabara eneo bunge hilo.
Alipokea habari za kuwepo kwa njama ya kumdhuru baada ya mmoja wamarafiki zake kumfichulia kuhusu mazungumzo yaliyofanywa na wafanyakazi wa CDF afisi ya Kesses.
Alilazimika kuandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Eldoret Central akiandamana na wakili wake Jonah Kirwa.
Wanyama alisema alipokea vitisho hivi muda mfupi baada ya kufanya taarifa hiyo na alilazimika kuandikisha taarifa ya kujieleza kuhusu hatua hiyo.
Alisema alipokea habari za kuwepo kwa njama ya kumdhuru baada ya mmoja wamarafiki zake kumfichulia kuhusu mazungumzo yaliyofanywa na wafanyakazi wa CDF afisi ya Kesses.
"Niliamua kupiga ripoti kwa sababu hii sio mara ya kwanza natishiwa maisha na watu wanaohisi kukwaruzwa na utendakazi wangu kama mwandishi wa habari," Wanyama alisema.
Wanyama alianza kupokea vitisho muda mfupi baada ya kufanya taarifa hiyo na akalazimika kuandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Eldoret Central akiandamana na wakili wake Jonah Kirwa.