This archive report was first published on 26 June 2020.
Idadi ya maambukizi ya coronavirus nchini Kenya imeongezeka kwa kasi baada ya watu 149 kupatwa na virusi vya ugonjwa huo chini ya saa 24 zilizopita.
Watu hao 149 ni Wakenya, huku mmoja wao akiwa ni rais kutoka nje, na walipatikana na ugonjwa huo baada ya sampuli 3,090 kufanyiwa ukaguzi.
Watu hao wameongezwa kwa idadi ya maambukizi ya coronavirus nchini Kenya, ambayo sasa imeongezeka hadi watu 5533, kwa mujibu wa katibu msimamizi wa wizara ya Afya, Rashid Aman.
Watu 5 pia wamefariki kutokana na ugonjwa huo, na idadi ya vifo kuongezeka hadi watu 137.
Visa vya maambukizi vimeongezwa kwa kaunti za Nairobi na Mombasa, ambazo ziliongoza kwa visa 73 na 20, mtawalia.
Wizara ya Afya pia imepokea mchango wa maski kutoka kampuni kadhaa katika vita vya kupambana na makali ya covid-19.
Idadi ya maambukizi ya coronavirus nchini Kenya imeongezeka kwa kasi baada ya kisa cha kwanza kurekodiwa mwezi Machi.