This archive report was first published on 26 June 2020.
Wakati Raila Odinga anaendelea kupata nafuu katika hospitali ya German nchini Dubai, Gavana wa Mombasa Hassan Joho amewahakikishia Wakenya kuwa kiongozi huyo wa chama cha ODM anaendelea kupata nafuu na atarejea nchini hivi karibuni.
Oburu Oginga, kakake wa Raila, alithibitisha kuwa Raila alisafirishwa hadi Dubai Jumapili, Juni 21 kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kwenye mgongo wake.
Gavana Joho alisema alizungumza na Raila na yuko buheri wa afya. "Nilizungumza na kiongozi wetu wa chama cha ODM, nafurahia na kuwa na matumaini kuwa anaendelea kupata nafuu, sisi kama wanachama wa ODM tunamtakia afueni ya haraka," Joho alisema.
Wakenya mitandaoni pia wamemtakia afueni ya haraka kiongozi huyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.