This archive report was first published on 26 June 2020.
Video ya Mbunge wa Sirisia John Waluke akikiri kuhusu yeye na wenzake kupokea hongo bungeni imeibuka mtandaoni.
Waluke alipatikana na hatia ya kuitapeli Bodi ya Nafaka na Mazao nchini (NCPB) KSh 297 milioni aliagizwa kulipa KSh 727 milioni au afungwe miaka 7 gerezani.
Alisema amepokea mlungula mara kadhaa ya kati ya KSh 100,000 na KSh 200,000 kulingana na kazi ambayo anatakiwa kuifanya.
"Sisi sote tumepokea kitu, tunaopaswa kuwa wakweli...nyakati zingine zingine tunapokea KSh 100,0000 ama KSh 200,000, inalingana....kwani wewe unaweza kukataa pesa? Ni Mungu hawezi kubali," alisema.
Waluke aliyatoa matamshi hayo baada ya kuibuka ripoti kwamba wabunge walipokea hongo ili kuuangusha mswada kuhusu sukari ya kutoka nje ya nchi.