Skip to main content

Washukiwa walionaswa na CCTV wakiiba kimabavu wasakwa na DCI

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 25 June 2020.

Washukiwa walionaswa na CCTV wakiiba kimabavu wasakwa na DCI

Video iliibuka mtandaoni Alhamisi, Juni 25, 2020, ikimuonesha jamaa akiibiwa kimabavu mchana.

Washukiwa waliomshambulia jamaa walimpokonya kila alichokuwa nacho na kuhepa.

Idara ya Upelelezi (DCI) imeanzisha uchunguzi wa kina dhidi ya kisa hicho.

Maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wameanzisha uchunguzi dhidi ya video iliyosambaa mtandaoni iliyomuoenesha jamaa akiibiwa kimabavu mchana peupe.

Picha za CCTV zilinasa tukio hilo Alhamisi, Juni 25, 2020, wakati jamaa alikuwa akielekea kazini.

Aliyesambaza video hiyo alisema kisa hicho kilitokea karibu na Ubalozi wa Thai, mtaani Kilimani.

Video hiyo inaonyesha jamaa akiandamwa na jamaa wawili waliokuwa wamevalia jeketi za kofia.

Jamaa huyo alionekana kugutushwa baada ya mmoja wa watu hao kumtishia na bunduki kabla ya kuanza kumpekua mifukoni.

Idara ya DCI ilisema imeanzisha uchunguzi dhidi ya kisa hicho na washukiwa watakamatwa karibuni.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →