This archive report was first published on 25 June 2020.
Matukio muhimu ya wiki hii ¶
Wakati wa wiki hii, matukio mengi yamegonga vichwa vya habari. Kati ya mambo muhimu, Gavana Anne Mumbi Waiguru Jumatano, Juni 24, aliambia kamati teule ya seneti kuwa alitimuliwa kwa sababu ya kuunga mkono ripoti ya BBI.
Waiguru alisema hakuna ushahidi ambao uliwasilishwa mbeleya kamati hiyo na kwa hivyo ni siasa za kitaifa.
Runinga ya K24 ambayo inamilikiwa na shirika la utangazaji la Media Max imewafuta kazi ghafla wafanyakazi zaidi ya 100.
Wafanyakazi waliopigwa kalamu wamekuwa wakifanya kazi katika shirika hilo, ikiwa ni pamoja na mtangazaji Nancy Onyancha na mumewe Joab Mwaura.
Waiguru alikuwa akicheza mchezo wa kadi almaarufu 'Solitaire' kwenye simu yake wakati kesi dhidi yake ya kumfurusha mamlakani ilipokuwa ikisikizwa katika bunge la seneti.
Aliyekuwa waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri amesajili chama chake cha kisiasa tayari kwa mirindimo ya 2022.
Wanamziki Betty Bayo Jumapili, Juni 21 aliwasisimua wanamtandao baada ya kumtumia aliyekuwa mumewe mhubiri Victor Kanyari ujumbe wenye utani siku ya kusherekea kina baba.