This archive report was first published on 25 June 2020.
Polisi wamewakamata watu 64 wanaodaiwa walijaribu kuwahonga polisi wanaoshika doria katika kizuizi cha Blue Post mjini Thika, kaunti ya Kiambu.
Watu hawa walikuwa wakijaribu kuvuka kizuizi hicho ili kuingia kaunti ya Murang'a, lakini walikamatwa na polisi.
Waliokamatwa ni madereva 16 na abiria 48 waliosafiri kutoka Nairobi.
Maafisa wa polisi waliosemekana kuwasaidia wasafiri walionywa huku adhabu kali ikitangazwa kutolewa watakaonaswa wakivunja sheria.
Maagizo ya kuingia na kutoka jijini Nairobi na viunga vyake yilitangazwa na Rais Uhuru Kenyatta kutokana na kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya coronavirus nchini.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alitangaza kuwa baadhi ya watu wanapuuza maagizo hayo na kutumia njia mbadala kupenyeza nje na ndani ya jiji la Nairobi.