Skip to main content

Mshukiwa wa Wizi wa Kimabavu Aliyeachiliwa 'Kimakosa' Asakwa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 25 June 2020.

Mshukiwa wa Wizi wa Kimabavu Aliyeachiliwa 'Kimakosa' Asakwa

Polisi wamsaka mhalifu sugu ambaye aliachiliwa 'kimakosa' baada ya kutumia ujanja wa majina.

Alipokamatwa kwa tuhuma za wizi wa kimabavu, mshukiwa Peter Kamau Nginge alikuwa na jina sawa na la mfungwa mwingine aliyekamatwa kwa kosa linalohusiana na pombe.

Wakati kesi ikiendelea, Kamau alijifanya kuwa mshukiwa aliyekamatwa kuhusiana na kosa la pombe, na ndipo aliachiliwa huru pasi na polisi kugundua ujanja wake.

Alipokuwa na kesi iliyopaswa kuamuliwa Juni 27, 2020, Kamau alitumia fursa ya kufanana kwa majina na mfungwa mwingine kuhepa gerezani.

Alitajwa kama mhalifu sugu ambaye ametekeleza wizi wa kimabavu hususan katika barabara kuu 2018.

Maafisa wetu wanamsaka na ni tumaini langu atakamatwa hivi karibuni, alisema Kamanda wa Polisi mjini Naivasha, Samuel Waweru Jumatano, Juni 24.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →