This archive report was first published on 24 June 2020.
Gerishon Kamotho, mkulima mmoja wa mahindi katika kaunti ya Nakuru, alikuwa na hasara kubwa baada ya mimea yake ya mahindi kuharibiwa na maji ya mvua ya mwaka jana.
Alisema kuwa alitumia zaidi ya shilingi elfu thelathini (30,000) wakati wa upanzi wa mahindi, na kuwa na hasara ya shilingi elfu thelathini (30,000) baada ya mimea yake kuharibiwa.
"Mimea ya mahindi ilikuwa imemea na kunawiri vizuri, lakini baada ya wiki chache baada ya kumea, nilizinyunyizia dawa ya magugu na wadudu wanaovamia mimea huku nikitumia fedha zaidi," akasema Kamotho.
Alisema kuwa alikuwa na matumaini kwamba mvua itapungua, lakini ilikuwa na madhara makubwa shambani.
Wakulima wengi wamepata hasara kubwa tangu mvua kubwa ilipoanza kunyesha wiki chache zilizopita.
Bi Jane Wanjiru, mkulima mmoja, alisema kuwa anatembea mara kwa mara katika maonyesho ya kilimo na semina zinazo husiana na kilimo ambapo wakulima hupata maarifa na ujuzi mwingi.
"Shamba langu liko mahali ambapo sio sawa, lakini nimepanda nyasi kwa mpangilio ili kuzuia mmomonyoko wa udongo mvua kubwa inaponyesha," akasema Wanjiru.
Wakulima wengi huhimizwa kupanda miti au matunda shambani mwao ili kuzuia mafuriko kama hayo yanayo haribu mimea yao.