Skip to main content

Ukuzaji Nyanya: Bi Njuguna Anapata Mapato Mazuri

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 24 June 2020.

Bi Margaret Nyambura Njuguna, mkulima mdogo wa nyanya, anapata mapato mazuri kutokana na ukuzaji wa nyanya kwa kutumia nyumba ya vioo.

Alipanda nyanya kwa nafasi ya 45cm kwa 60cm na kutumia miche 450 iliipanda.

Alipata shilingi elfu tano (5,000) kwa kila kreti aliyouza.

Bi Njuguna alianzisha chumba cha vioo cha mita sita kwa nane mwaka wa 2018 na kutumia shilingi elfu arobaini (40,000) katika matumizi ya ujenzi, mbolea na mbegu za kupanda.

Alisema kuwa kukuza nyanya katika chumba cha vioo husaidia kwa hali ya kiuchumi na pia kukinga mimea kutoka kwa jua kali na mvua kubwa inaponyesha.

Alisema kuwa ndani ya chumba hiki, nuru ya jua na maji ya mvua ya kiwango cha chini ndio huhitajika.

Bi Njuguna alisema kuwa yeye hupata kati ya shilingi elfu tano (5,000) na shilingi elfu sita (6,000) kwa wiki moja katika sehemu yake ndogo aliyoipanda nyanya.

Alisema kuwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo ambayo alizipanda nyanya, Bi Njuguna anakumbuka vile alipata shilingi elfu sabini (70,000), pesa nyingi ambazo aliwahizipata tangu mwaka wa 2018 alipoanza kupanda Anna F-1.

Alisema kuwa ingawa kulika virusi vya Covid-19 Machi mwaka huu, hakuathirika sana kwa vile mauzo yake alikuwa akiiuza kwa soko la ndani.

Alisema kuwa mauzo yake imeongezeka tangu ugonjwa huu wa Corona ulipofika nchini.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →