Skip to main content

Afisa wa Polisi Aliyedaiwa Kumuua Mkewe Aachiliwa Kwa Dhamana

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 23 June 2020.

Polisi Kennedy Otieno Oloo aliyeshukiwa kumuua mkewe Leah Nasuhu Terewa aachiliwa kwa dhamana ya KSh 500,000 na mahakama ya Nakuru mnamo Juni 23, 2020.

Jaji Rachael Ngetich alimwachilia Oloo kwa dhamana na mdhamini wa kiasi sawia na hicho baada ya kukana mashtaka ya kumuua mkewe kulingana na ripoti ya Daily Nation.

Alidaiwa kutekeleza uhayawani huo mnamo Juni 11, 2020 nyumbani kwao Kiamunyeki, Nakuru Mashariki.

Alikamatwa Juni 17 baada ya upasuaji wa maiti kuonesha Terewa alinyongwa.

Alidai mkewe alijitia kitanzi nyumbani mwao baada ya mzozo wa nyumbani.

Jaji Ngetich aliagiza smhukiwa azuiliwe katika jela ya Nakuru.

Walitokea kizaa zaa katika makafani ya hospitali ya Evan Sunrise baada ya jamaa za Terewa kuupigania mwili wake.

Wakili wa familia ya Terewa, Lewin Omollo, alisema ilibidi mahakama iingiliekati ndiposa Oloo aipe familia ya marehemu stakabadhi za kuuondoa mwili wake katika makafani na kumzika.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →