Skip to main content

Ugonjwa wa COVID-19 wavamia makambi ya kijeshi nchini Kenya

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 22 June 2020.

Ugonjwa wa COVID-19 wavamia makambi ya kijeshi nchini Kenya

Wanajeshi 80 wametengwa katika kambi ya Kabete baada ya kupatwa na COVID-19.

Maafisa wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya walichukua hatua za haraka za kuzuia kuenea kwa virusi hivyo baada ya watatu wa wanajeshi kutoka kambi ya Embakasi, jijini Nairobi, kuambukizwa virusi hivyo.

Idadi kubwa ya wanajeshi walihamishwa kutoka kambi ya Embakasi hadi Kahawa kama njia ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Visa vya awali vya COVID-19 vilithibitishwa katika makambi ya jeshi, na kituo cha kujitenga kilibuniwa Embakasi, lakini wakati idadi iliongeza ilihamishwa hadi kambi ya Kabete ambayo iligeuzwa kituo cha matibabu cha wanajeshi.

Wanajeshi ambao walikuwa likizoni wakiagizwa wasirejee kazini kwani hakuna anayeruhusiwa kuingia katika majengo hayo.

Visa jumla vilivyothibitishwa nchini ni 4,738, vifo 123 huku 1,607 wakipata nafuu.

Maafisa wengi kambini hutumia muda mwingi nje ya majengo hayo huku wengi wao wakiwa na makazi yao katika maeneo ya Kahawa Sukari, Kahawa Wendani na Githurai.

Kituo cha kambi ya Kabete sasa kinachukua wanajeshi 80 waliotengwa baada ya kupatwa na COVID-19.

Visa vya awali vya COVID-19 vilithibitishwa katika makambi ya jeshi, na kituo cha kujitenga kilibuniwa Embakasi, lakini wakati idadi iliongeza ilihamishwa hadi kambi ya Kabete ambayo iligeuzwa kituo cha matibabu cha wanajeshi.

Visa jumla vilivyothibitishwa nchini ni 4,738, vifo 123 huku 1,607 wakipata nafuu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →