Skip to main content

Naibu Rais William Ruto Kipaumbele Katika Magazeti Ya Jumatatu, Juni 22

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 22 June 2020.

Naibu Rais William Ruto Kipaumbele Katika Magazeti Ya Jumatatu, Juni 22

Naibu Rais William Ruto amepewa kipaumbele katika magazeti ya Jumatatu, Juni 22, huku washirika wake wengi wakiapa kutohudhuria mkutano wa Kundi la Wabunge wa Chama cha Jubilee.

Washirika wa Ruto wameapa kutohudhuria mkutano wa Kundi la Wabunge wa Chama cha Jubilee ambao utaongozwa na Rais Uhuru asubuhi ya leo, macho yote yakimulekezea Ruto.

Wengi wana hamu ya kujua endapo Naibu Rais atahudhuria mkutano ambao ajenda yake ni kubaini hatma ya baadhi ya wandani wake ikiwemo ya Kiongozi wa Wengi Bunge la Kitaifa Aden Duale ambaye huenda atapoteza kiti chake.

Chama Cha Raila Odinga Na Wiper Vinatazamiwa Kuvuna Unono

Chama cha Raila Odinga na Wiper vinatazamiwa kuvuna unono kufuatia ushirikiano wa wawili hao na Rais Uhuru.

Chama hicho hiki huenda wanachama wao wakawa miongoni mwa watakaorithi nyadhifa 16 za wandani wa Ruto ambao waliadhibiwa.

Inspekta Jenerali Hillary Mutyambai Atakuwa Akiwasiliana Na Wananchi Moja Kwa Moja Kupitia Twitter

Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai ametangaza kuwa atakuwa akiwasiliana na wananchi moja kwa moja kupitia Twitter kila Jumatatu.

Wananchi watatumia fursa hiyo kumfahamisha Mutyambai kuhusu changamoto zao na kile wanahisi kinatakiwa kufanywa ili kuboresha huduma ya polisi.

Gavana Mutua Akashifu Vyama Vya Kisiasa Vilivyobuni Serikali Ya Mseto

Gavana wa Machakos, Alfred Mutua alikosoa hatua ya baadhi ya vyama vya kisiasa ya kubuni serikali ya mseto kwa kuitaja kama ya kikabila na isiyokuwa na ajenda yoyote ya maendeleo.

Mutua alisema hana nia yoyote ya kuungansha chama chake cha Maendeleo Chap Chap katika mrengo wowote ambao hauna haja ya kutimiza mahitaji ya watu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →