Skip to main content

Rais Trump Kampeni ya Kwanza baada ya Corona: Idadi ndogo ya wafuasi

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 21 June 2020.

Rais Trump Kampeni ya Kwanza baada ya Corona: Idadi ndogo ya wafuasi

Ikizingatiwa kwamba nchi hiyo ilipoweka amri ya kutotoka nje kutokana na chimbuko la virusi vya corona, Rais wa Marekani Donald Trump amefanya kampeni yake ya kwanza baada ya mkurupuko huo.

Alipofanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara, Rais Trump alikuwa mbele ya watu wachache kinyume na umati mkubwa wa watu uliokuwa unatarajiwa kufurika katika uwanja huo.

Alijigamba kuwa karibia watu milioni moja walikuwa wameomba tiketi ya kuhudhuria mkutano huo ulioandaliwa eneo la benki ya Tulsa katika kituo cha Oklahoma, lakini viti 19,000 vya uwanja huo vilisalia wazi bila watu na mipango yake ya kuhutubia watu ambao wangelazimika kukaa nje kwa sababu ya uwanja kufurika ilisalia ndoto.

Alipohutubia umati mdogo kinyume na alivyotarajia mamilioni kufurika, Rais Trump aliguzia suala la virusi vya corona nchini humo ambapo alizua mzaha kuwa aliwaambia maafisa wa afya wapunguze upimaji wa virusi hivyo kwani watu wengi wanaugua.

Alisema, "Huu ndio ubaya: Unapofanya vipimo kwa kiasi kile, utawapata watu wengi, utapata visa vingi vya corona, aliuambia umati wa wafuasi wake uliomshangilia.Kwa hivyo nikasema 'punguza kasi ya kupima.Walipima na wakapima,'".

Waliohudhuria mkutano mkutano huo walilazimika kutia saini mkataba wa kuilinda timu ya kampeni ya Trump na haitawajibika na ugonjwa wowote iwapo watapata maambukizi.

Ikizingatiwa kwamba zaidi ya watu milioni 22 wanaugua ugonjwa huo huku 119,000 wakipoteza maisha yao, kampeni za Trump za kuwania urais kwa mara ya pili zilikua ndio mkusanyiko mkubwa zaidi wa watu katika wakati Oklahoma inashuhudia ongezeko la visa vya corona vilivyothibitishwa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →