This archive report was first published on 21 June 2020.
Waziri Kagwe Aomba Msamaha Kwa Waliowekwa Karantini ¶
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema watu 260 wamepatawa na virusi vya coronavirus na kufikisha idadi ya maambukizi kuwa 4738.
Waziri huyo alisema hayo Jumapili Juni 21 huku kaunti za Nairobi na Mombasa zikiendelea kurekodi idadi ya juu ya maambukizi.
Watu wawili pia wameripotiwa kufariki kutokana na maambukizi hayo chini ya saa 24 zilizopita.
Waziri Kagwe alisema serikali imeweza kujifunza mengi ndani ya siku 100 tangu coronavirus ifike humu nchini.
Alisema sasa watakaopatwa na virusi watakuwa wanaruhusiwa kukaa nyumbani kuendelea kupata nafuu.
Alisema wanaolazwa hospitali watakuwa wanaruhusiwa kurudi nyumbani baada ya siku 14 kwa sababu watakuwa bila hatari ya kuambukiza wengine.
Waziri Kagwe amewataka Wakenya kuendelea kupigana na covid-19.
Alisema hayo Jumapili Juni 21 huku kaunti za Nairobi na Mombasa zikiendelea kurekodi idadi ya juu ya maambukizi.
Waziri huyo pia aliomba msamaha kutoka kwa Wakenya kwa jinsi walivyofanyiwa siku za kwanza za ripoti ya covid-19.
Alisema hayo Jumapili Juni 21 huku kaunti za Nairobi na Mombasa zikiendelea kurekodi idadi ya juu ya maambukizi.