This archive report was first published on 21 June 2020.
Naibu Mwenyekiti wa Jubilee David Murathe ameonya wabunge wa Jubilee dhidi ya kususia kikao kilichoitishwa na kiongozi wa chama Jumatatu, Juni 22.
Alisema yeyote atayejaribu kukosa kikao hicho awe tayari kwa hatua za kinidhamu kama walivyofanyiwa maseneta hapo awali.
Wabunge wa Jubilee walipokea ujumbe Jumamosi, Juni 20 wakialikwa kwenye kikao hicho katika ukumbi wa KICC.
Alisema baadhi ya wanachama wamekuwa na ukosefu wa nidhamu kwa uongozi wa chama na hilo halitakubalika.
Aliongeza, "Tumekuwa tukishuhudia ukosefu wa uaminifu kwa chama, kutotii na hata matusi kwa kiongozi wa chama. Hayo lazima yafike mwisho," alisema Murathe.
Wabunge wa Jubilee watafanya mkutano wa kwanza katika ukumbi wa KICC Jumatatu, Juni 22, na Rais Uhuru Kenyatta ataongoza kikao hicho.
Naibu Mwenyekiti wa Jubilee David Murathe alitoa onyo kwa wabunge wa Jubilee wasikose kuhudhuria kikao cha Jumatatu, Juni 22.