Skip to main content

Njia 10 Rahisi za Kuondoa Weusi kwenye Kisugudi cha Mkono

N

Nyakundi Report

Newsroom 3 min read

This archive report was first published on 21 June 2020.

Uweusi kwenye kisugudi cha mkono ni tatizo la kawaida ambalo linaweza kusababishwa na mkusanyiko wa seli zilizokufa kutokana na msuguano sehemu hizo.

Wakati wa kukutanisha goti lako na kisugudi wakati unapofua, au shambani, ule msuguano hufanya ngozi yako katika maeneo hayo iwe nyeusi.

10. Tango

Tango ina uwezo mkubwa katika kuifanya ngozi kuwa nyeupe. Ina uwezo mkubwa wa kuzuia ngozi kuharibika na vitamini A na C ambavyo ni muhimu sana katika kuiboresha ngozi na kuifanya iwe laini tena.

Changanya tango na limao kabla ya kuupaka kwenye goti au kisugudi na maeneo meusi unayotaka yawe meupe.

9. Ndimu na magadi

Ndimu ina uwezo mkubwa wa kuzuia ngozi kuharibika na vitamini C ambavyo ni muhimu sana katika kuiboresha ngozi na kuifanya iwe laini tena.

Changanya ndimu na magadi kiasi katika sehemu zenye weusi na tulia kwa muda wa saa moja kisha usha sehemu hiyo.

8. Mshubiri na maziwa

Unachotakiwa kufanya ni kupaka mchanganyiko wako kwenye sehemu yenye weusi na uache kwa nusu saa hivi au hata usiku mzima na ioshe sehemu hiyo kwa maji ya joto kiasi kabla ya kuipa mafuta ya kulainisha au moisturiser.

7. Kiazi

Kiazi kina kimeng’enya ambacho kinasemekana kuwa na uwezo mkubwa wa kundoa uweusi kwenye ngozi bila ya kuongeza chochote.

Changanya kiasi cha kisazi na maji ya joto kiasi kabla ya kuupaka kwenye goti au kisugudi na maeneo meusi unayotaka yawe meupe.

6. Njano na maziwa

Njano pia ina uwezo mkubwa wa kupambana na madini melanin ambayo ndicho chanzo cha ngozi nyeusi hasa katika maeneo niliyotaja.

Changanya njano na maziwa ili kuwa na mchanganyiko bora na upaka kwenye goti au kisugudi na maeneo meusi unayotaka yawe meupe.

5. Mafuta ya mnazi

Mafuta kutokana na tunda hili yana vitu mihimu vyenye faida sana hasa vitamini E ambayo husaidia katika kurekebisha seli za ngozi zilizokufa au kuharibika.

Upaka mafuta hayo kwenye goti au kisugudi na maeneo meusi unayohisi ni maeusi sana na yanahitaji kufanywa kuwa meupe.

4. Asali

Wanasema waliowahi kuutumia mchanganyiko wa asali na limao kuwa bora zaidi katika kuifanya ngozi yako kuwa nyororo hasa katika maeneo yenye ngozi iliyokauka na seli zilizokufa.

Changanya asali na limao na upaka kwenye goti au kisugudi na maeneo meusi unayotaka yawe meupe.

3. Sukari na mafuta ya zaituni

Mchanganyiko wa sukari na mafuta ya zaituni utakusaidia kuimarisha ngozi yako na hata kuondoa seli zilizokufa kwenye magoti na mikono.

Changanya sukari na mafuta ya zaituni na upaka kwenye goti au kisugudi na maeneo meusi unayohisi ni maeusi sana na yanahitaji kufanywa kuwa meupe.

2. Shayiri

Shayiri pia ni kifaa kizuri katika kuimarisa ngozi yako. Unahitaji limao na chumvi katika kuufanya mchanganyiko unaofaa au bora.

Changanya shayiri na limao na upaka kwenye goti au kisugudi na maeneo meusi unayotaka yawe meupe.

1. Siki na maziwa mgando

Mchanganyiko wa asidi aina ya acetic katika siki na lactic katika maziwa mgando utafanya ngozi katika goti au kisugudi kuwa nyororo na ya kuvutia.

Changanya siki na maziwa mgando na upaka kwenye goti au kisugudi na maeneo meusi unayotaka yawe meupe.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →