Skip to main content

Mkutano wa Wandani wa DP Ruto Ufanywa Kwa Ufupi na Polisi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 20 June 2020.

Naibu Rais William Ruto alikuwa akitarajiwa kuhudhuria mkutano wa wandani wa DP Ruto uliofanyika nyumbani kwa mbunge wa Malava Malulu Injendi, Juni 19, 2020.

Maafisa wa polisi walijihami na kufyatua vitoa machozi kwa watu waliokuwa wakikusanyika, huku wabunge kadhaa kutoka eneo la Magharibi mwa Kenya walikuwa wahudhurie kikao hicho.

Seneta wa Kakamega Bonny Khalwale na wabunge wa mrengo wa chama cha Amani National COalition pia walikuwa wahudhurie kikao hicho.

Maafisa waliotumwa walijihami na kufyatua vitoa machozi kwa watu waliokuwa wakikusanyika, huku wabunge walilazimika kuingia mitini kuepuka maafisa wa polisi.

Video iliibuka ya mbunge wa Kimilili Didmus Barasa akijaribu kuteta kwa maafisa wa polisi kuruhusu mkutano huo kuendelea mradi maagizo kuhusu kukabili COVID-19 yazingatiwe.

Maandalizi yaliyokuwa yamefanywa nyumbani kwa mbunge wa Malava. Picha: Ombati

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →