This archive report was first published on 20 June 2020.
Moses Kuria: Uhuru Kenyatta Hatampigia Debe Mgombea Yeyote 2022 ¶
Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amesema Rais Uhuru Kenyatta hatamuunga mkono mgombea yeyote wa urais baada ya hatamu yake kumalizika 2022.
Matamshi ya Kuria yanajiri wakati wengi wamezua gumzo kwamba huenda rais anapanga kikosi chake ambacho atakiunga mkono atakapoondoka mamlakani.
Alisema hili baada ya Uhuru kutangaza kuwa hatasalia mamlakani hatamu yake itakapokamilika.
"Nimekuwa nikishikilia kuwa Uhuru Kenyatta ni mwanademokrasia. Hatasalia mamlkani wala kuwajaribu kukalia kiti cha Waziri Mkuu. Ataondoka na kuelekea nyumbani kwa heshima ifiakiapo 2022. Hatamuunga mkono mgombeaji yeyote," aliandika Uhuru kwenye Twitter Alhamisi, Juni 18.
Matamshi ya Kuria yanajiri baada ya kuibuka semi kwamba rais anaandaa kikosi ambapo baadaye atampendekeza mmoja kati yao atakayemuunga mkono muda wake ukikamilika.
Uhusiano kati ya Uhuru na Naibu Rais William Ruto umekuwa ukididimia kila kuchao huku wengi wakihusisha hatua hiyo kutokana na urafiki wake na Kinara wa Upinzani Raila Odinga.
Uhuru na Raila wamekuwa rafiki wa karibu tangu Machi 9, 2018 wakati wa salamu za maridhiano.