This archive report was first published on 19 June 2020.
Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amepuuza ripoti kwamba mrengo wa Naibu Rais William Ruto utajiondoa ndani ya chama cha Jubilee.
Alisema hilo kwa sababu wao ni baadhi ya walioijenga Jubilee na hivyo lazima wapate matunda yake.
Alisema hayo Ijumaa, Juni 19, baada ya habari kuenea kwenye mitandao kuwa DP Ruto anaunda chama chake.
"Puuzeni porojo zinazoenezwa. Chama cha Jubilee ndicho chama chetu, kazi ya mapenzi yetu na marengo yetu ambacho tunasubiri matunda yake," alisema Murkomen.
Alieleza kuwa afisi za Jubilee Asili ni mahali tu pa wanachama wao kukutana ili kupanga siasa yao.
Alisema pia kuwa Jubilee Asili Centre ni mahali pa wanachama walionyimwa nafasi ya kuingia katika afisi cha chama kukutana.
Alisema hilo baada ya ripoti za kuwepo kwa mikakati ya Ruto kujenga nyumba yake mpya ya siasa zilijiri Alhamisi, Juni 18 alipokutana na kundi la wabunge katika afisi hizo.