This archive report was first published on 19 June 2020.
Polisi aliyekashifiwa kwa kumpiga risasi na kumuua mvulana Yassini Moyo mtaani Huruma Machi mwaka huu alikuwa na dalili za virusi vya ugonjwa wa corona.
Wakili wa Duncan Ndiema aliarifu mahakama kuwa mteja wake alikuwa ameonyesha dalili za virusi vya ugonjwa wa corona na alikuwa amefika katika hospitali ya Mbagathi kufanyiwa vipimo.
Alionyesha dalili za kuwa na virusi vya ugonjwa wa corona, na hivyo kuibua wasiwasi kuhusu matibabu yake.
Upande wa mashtaka umesema iwapo mshukiwa atapatikana na virusi, serikali itagharamia matibabu yake lakini lazima ajibu mashtaka dhidi yake.
Hakimu Daniel Ogembo ameagiza shirika la IPOA kuchunguza hali ya kiafya ya mshukiwa na afikishwa mahakamani na matokeo baada ya kufanyiwa vipimo.