This archive report was first published on 19 June 2020.
Chama cha watu wasioamini Mungu yupo, (AIK) kimefutilia mbali pendekezo la waziri wa Elimu George Magoha la kutaka sinema za ngono zipigwe marufuku Kenya.
Badala yake, kiongozi wa chama hicho Harrison Mumia ametaka masomo kuhusu ngono salama yazinduliwe shuleni.
Waziri Magoha alipendekeza kuwa video za ngono zinachangia pakubwa mimba za mapema, na alisema atamshawishi rais Uhuru Kenyatta pamoja na mawaziri wenzake kubadilisha sheria ili izuia sinema zote zinazohusisha ngono.
Madai kuibuka kuwa zaidi ya wasichana 4,000 wamepachikwa mimba za mapema kati Januari na Mei mwaka huu.