Skip to main content

Magavana na Wafanyakazi 66 Wanasakwa baada ya COVID-19 Kupiga Hodi Ikulu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 19 June 2020.

Ikulu ilikuwa na shida kubwa baada ya wafanyakazi wanne wa ikulu kupatikana na virusi vya COVID-19 mapema wiki hii.

Maafisa wa afya wanataka magavana hao waliohudhuria mkutano wa baraza la mawaziri Juni 10, katika Ikulu wafanyiwe vipimo vya virusi hivyo.

Magavana waliohudhuria mkutano ikulu kufanyiwa vipimo vya COVID-19, ikijumuisha naibu Rais William Ruto, wakati Rais Uhuru Kenyatta na familia yake hawakupatikana na virusi hivyo.

Imebainika kuwa Rais Uhuru Kenyatta amefutulia mbali mkutano mwingine wa maafisa wa kaunti ambao ulikuwa ufanyike hii leo Ijumaa, Juni 19, katika ikulu akihofia maambukizi zaidi.

TUKO.co.ke inafahamu kuwa wafanyakazi wanne wa ikulu waliopatikana na COVID-19 wametengwa katika hospitali ya chuo kikuu cha Kenyatta ambapo pia wanapokea matibabu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →