Skip to main content

Gavana Sonko Amsaidia Mwenye Umri wa Miaka 75 Alipokuwa Kwenye Uchochote

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 18 June 2020.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amejitokeza kumsaidia kocha wa zamani wa timu ya kitaifa ya kandanda ya Kenya, Marshall Mulwa, ambaye alikuwa akiishi maisha ya uchochote baada ya familia yake kuamua kuishi ughaibuni.

Maisha ya uchochote ya Mulwa yalikuwa ya kujisikia baada ya TUKO.co.ke kutoa taarifa kuhusu maisha yake ya uchochote aliyokuwa akiishi mtaani Kitengela, kaunti ya Kajiado.

Wakati kikosi cha Sonko kilimtembelea katika nyumba yake ya kukodisha, Mulwa alipokea chakula huku Sonko akiahidi kusaka njia zingine mwafaka zitakazomfaa ili kuboresha maisha yake.

"Mpira wa miguu unachukua jukumu muhimu katika jamii yetu kwa kuunganisha nchi yetu na pia kwa kuwapa vijana fursa ya kupata riziki," Sonko alibaini katika chapisho lake la Facebook.

Wakati akiwa nahodha wa kikosi cha Stars, timu hiyo ilipata ushindi mara tatu katika Cecafa Senior Challenge kati ya mwaka wa 1981 hadi 1983.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →