This archive report was first published on 18 June 2020.
Waziri wa Elimu George Magoha amesema kuwa sinema za ngono zinazoonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii ni kichocheo kikubwa cha mimba za mapema miongoni mwa wasichana haswa wenye umri wa chini ya miaka 19.
Alisema hili akiwa mjini Nakuru Alhamisi, Juni 18, 2020.
Magoha amesema atamshawishi Rais Uhuru Kenyatta pamoja na mawaziri wenzake wazingatie kubadilisha sheria ili izuia sinema zote zinazohusisha ngono.
Alisema kuwa sio lazima ziwe sheria za Kenya pekee, kwani nchi kadhaa za Afrika zimepiga marufuku tuvuti zinazoonyesha video hizo.
Magoha alitilia shaka madai kuwa idadi kubwa ya wasichana waliochini ya umri wa miaka 19 wamepachikwa mimba kati ya Januari na Mei mwaka huu.
Alisema atachunguza madai haya na kuuliza wasichana hao waliopata mimba wapi waliripoti kuwa wamepata mimba.
Magoha ameahidi kukabiliana vilivyo na wanaume watakaopatikana wakiwanyanyasa kijinsia watoto wa kike.