This archive report was first published on 18 June 2020.
‘Uuzaji wa mboga za kienyeji unalipa’ ¶
Ann Kinuthia, mama wa watoto wawili, alianza kuhisi athari za ugonjwa wa corona mwishoni mwa Machi 2020 na kwa kuwa lazima maisha yangesonga mbele, hakuwa na budi ila kuingilia biashara ya uuzaji wa mboga za kienyeji.
Alipoteza ajira katika kampuni ya Coca Cola, ambapo alikuwa mfanyakazi wa miaka minane, Ann alianza kuhisi kuwa uuzaji wa mboga za kienyeji ni njia bora ya kulea familia yake.
‘Baada ya kufanya hesabu, niliona biashara ya bidhaa za kula ndiyo bora kipindi hiki kwa sababu lazima watu wale,’ alisema Ann.
Alisema kuwa chaguo la mboga za kienyeji ni bora kwa sababu haliangusha na pia ni bora kwa kinga ya mwili.
‘Mboga ni kitoweo ambacho huliwa kila siku katika maboma ya familia nyingi nchini. Chaguo la mboga za kienyeji ni bora, watu wakizikumbatia ili kuimarisha kinga ya mwili,’ alisema Ann.
Alisema kuwa mapato yake ya siku ya kazi ni ya chini kuliko mapato yake ya zamani, lakini anasema kuwa anapata faida ya Sh800 kwa siku.
Shirika la Afya Duniani limeonya kuwa janga la Covid – 19 huenda likakawia kudhibitiwa, ikikumbukwa kwamba chanjo na tiba haijapatikana.
Ann anasema kuwa shabaha yake pia ni mkulima wa mboga za kienyeji.