This archive report was first published on 18 June 2020.
Video iliyosambaa mitandaoni inaonyesha utingo huyo akisakata densi huku akikusanya nauli kutoka kwa abiria wake.
Utingo huyo kutoka Tanzania alijiwachilia hadharani wakati wimbo wa Diamond Platnumz ulianza kuchezwa.
Alianza kusakata densi safari ilipokuwa ikiendelea pindi tu wimbo wa Diamond Platnumz ulianza kuchezwa redioni.
Aliweka kazi yake kando na kuanza kuzikwenda huku abiria waliokuwa ndani ya gari hilo wakisalia kuangua kicheko wakifurahia walichokiona.
Video hiyo ilisambazwa katika ukurasa wa Instagram wa Wasafi TV ambapo wengi walitoa maoni yao wakielezea tamaa yao ya kukutana na utingo huyo.