This archive report was first published on 17 June 2020.
Wakati wa mabadiliko ya Jubilee katika uongozi wake bungeni na seneti, wanne wa wandani wa Naibu Rais William Ruto walitimuliwa kutoka kamati za bunge walizokuwa wakihudumu.
Wanajumbe hao walioadhibiwa ni Cate Waruguru, Mbunge Moses Kuria, Cornelly Serem, na mwakilishi wa kina mama kaunti ya Bomet Joyce Chepkoech Korir.
Spika wa bunge alifahamishwa kuhusu hatua hii kupitia barua ya Kiranja mpya wa Jubilee katika bunge, Emmanuel Wangwe.
Wangwe alikuwa amewaandikia wajumbe hao akiwataka kujitetea wasitimuliwe na kuwapa siku saba kufanya hivyo.
Aliwajulisha notisi hiyo ikikamilika watakuwa hawatambuliwi tena kama wanakamati na chama chao cha Jubilee.
Wanajumbe hao walioadhibiwa walikuwa wafuasi sugu wa DP Ruto, lakini baada ya kubadili msimamo wao kisiasa, wameanza kurudi kwenye mrengo wa kisiasa wa handisheki unaomhusisha Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.