Skip to main content

Rais Magufuli kuwania muhula wa pili, aahidi maendeleo zaidi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 17 June 2020.

Uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 unatarajiwa kufanyika, na Rais wa Tanzania, John Magufuli, anaazimia kuwania tena kiti cha urais. Hii imethibitishwa baada ya Magufuli kuchukua fomu za kugombea muhula wa pili kutoka afisi ya chama chake cha CCM mkoani Dodoma.

Magufuli alipata fomu hizo takribani saa 24 baada ya kulivunja mbunge la 11 lililomaliza muda wake kulingana na katiba.

Alipovunja bunge hilo, Magufuli aliisifu serikali yake akidai imefanya juu chini kuhakikisha inatimiza ahadi ilizotoa alipokuwa akiomba kura mwaka wa 2015.

''Mabadiliko makubwa yamefanyika ikiwemo kuzuia utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi kwa kufungua masoko ya madini katika kila mkoa, ili kuongeza ushirikishwaji wachimbaji wadogo,'' Alisema Magufuli.

Ingawa Magufuli amekosolewa kwa masuala kadha wa kadha, ikiwemo kufanya maamuzi ya haraka, kuwafuta kazi baadhi ya mawaziri bali pia ameonyesha utendakazi wake kwa uwazi.

Magufulu ameahidi kufanya mengi zaidi endapo wananchi watampigia kura kwa muhula wa pili.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →