This archive report was first published on 17 June 2020.
Mwili wako haufai kuwa na sukari kupita kiasi, ina madhara makubwa ¶
Wakati tunapotafuta ladha ya sukari iliyokolea, baadhi yetu hupenda kuweka kiasi kingi kwenye vinywaji na vyakula vyetu na matokeo yake sisi hujikuta katika matatizo makubwa ya kiafya bila ya kujua kuwa chanzo ni sukari.
Yapo madhara mengi yatokanayo na mtu kupenda sana kutumia kiasi kikubwa cha sukari, baadhi yake ni uwezekano wa mtu kupatwa na unene wa kupindukia, hatari ya kupatwa na saratani, magonjwa ya moyo, chunusi, kisukari, matatizo ya meno na hata kudhoofika kwa ngozi.
Wakati tunapotumia kiasi kidogo cha sukari, kiwango cha juu cha sukari mwilini kunaweza kusababisha madhara makubwa. Kwa hivyo ni vyema kujiepusha na unywaji wa vinywaji, kama juisi na soda ambavyo huongezewa sukari ya ziada.
Wataalamu wa afya wanatueleza kwamba chupa moja ya soda huwa na wastani wa vijiko sita vya sukari, kiasi ambacho ni kikubwa mno kuliko kawaida. Kwa hivyo ni vyema kujiepusha na unywaji soda kupindukia ukidhani unakunywa kinywaji salama kwa kuwa hakina kilevi.
Wakati mtu anapoelewa kuhusu madhara ya sukari na lengo la kuiepuka ndipo atakapo kata shauri kupunguza kiwango anachotumia kwa siku. Hapa ni baadhi ya vidokezi vinavyoweza kukusaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa matumizi ya sukari:
- Fanya mazoea ya kusoma kiasi cha sukari kinachopatikana kwenye chakula au kinywaji chako.
- Kunywa kiasi kingi cha maji kila siku, na kuepuka unywaji wa pombe kupita kiasi.
- Kupata muda wa kutosha wa kupumzika ama kulala.