This archive report was first published on 16 June 2020.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza Juni 29, 2020 kuwa tarehe rasmi ya kufunguliwa kwa shule zote nchini humo.
Magufuli alipovunja bunge la 11 la Tanzania Jumanne Juni 16, 2020, alipongeza Watanzania kwa kuchukua tahadhari zinazohitajika kuhakikisha kuwa virusi vya COVID-19 havisambai kwa kasi.
''Namshukuru Mungu kwa kuliepusha taifa hili na virusi vya corona na nina washukuru viongozi wa dini kwa kuitika wito wa serikali kufanya maombi maalum ya kutuepusha na janga la corona,'' alisema Magufuli.
Magufuli pia alitangaza kuwa shughuli zote zilizositishwa kutokana na janga la ugonjwa wa corona zitarejeshwa katika hali ya kawaida.
Magufuli alidai kuwa ajira ya Watanzania imelindwa ipasavyo msimu huu wa mlipuko wa virusi vya corona na uamuzi wa kutofunga shughuli za uchumi ulikuwa sahihi.
Uchunguzi wa COVID-19 nchini Tanzania umeripoti visa 66 pekee vya maambukizi huku Kenya ikipanda kwa kasi na kufanya walioambukizwa kufikia 3,860.