This archive report was first published on 16 June 2020.
Naibu Rais William Ruto amekabiliwa na kashfa kubwa kutoka kwa mwakilishi wa wanawake wa Kaunti ya Laikipia Cate Waruguru, ambaye amesema kuwa Ruto sio kiongozi wa kusamehea kwa wepesi wanaomkosea, bali ni mtu mwenye kinyongo moyoni.
Waruguru alisema hivi kwa kujieleza kwa lugha ya Kikuyu, "William Ruto ni mtu ambaye sio mwepesi wa kusamehea, huonyesha hadharani kuwa mtu mwenye kinyongo moyoni, kwa hivyo mimi naonelea hafai kuwa rais," alisema.
Waruguru aliongeza kwa kusema kuwa Ruto anafaa kuchukua muda wake, na aige mambo kadhaa kutoka kwa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga iwapo anataka kuwa rais.
Ufichuzi huo wa Waruguru ulisababisha hisia mseto kutokana na wakenya kupitia mitandao ya kijamii, wengi wakimkashifu kwa kupotoshwa.