Skip to main content

Mwimbaji wa Benga, Omondi Long Lilo, Aaga Dunia

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 16 June 2020.

Mwimbaji wa Benga, Omondi Long Lilo, Aaga Dunia

Omondi Long Lilo, mwimbaji wa mtindo wa Benga, amekuwa akiugua saratani kwa muda na alifariki siku chache baada ya mwanamziki maarufu wa Ohangla, Abenny Jachiga.

Kifo chake kinakujia siku chache baada ya Abenny Jachiga, ambaye alikuwa akiugua saratani pia, kuaga dunia katika hospitali ya Kisumu.

Omondi Long Lilo alikuwa akiomba msaada wa kifedha kugharamia matibabu yake, na alikuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Bondo.

Mashabiki wa Omondi na wapenzi wa miziki ya Benga walijaa mtandaoni kutuma salamu zao za rambi rambi kwa familia.

Rafiki wake wa karibu, Jack Oduor, alithibitishia Tuko.co.ke kuwa Omondi alikata roho siku ya Jumanne, Juni 16, kinyume na habari zilizochapishwa kwenye mitandao jamii kwamba alifariki Juni 11.

Omondi Long Lilo alikuwa akiugua saratani kwa muda na alikuwa akiomba msaada wa kifedha kugharamia matibabu yake.

Staa huyo wa Benga anajiunga katika orodha ya Wakenya wengine ambao wamekuwa wakipambana na ugonjwa huo hatari ambao ni ghali kutibu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →