Mjusi Mkubwa Zaidi Duniani Amebainika Nchini China

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 18 September 2019.

Mjusi Mkubwa Zaidi Duniani Amebainika Nchini China

Utambuzi wa DNA wa mwanzoni ulisema kuwa mjusi huyo mkubwa alikuwa wa pekee ambaye ana ukubwa kiasi hicho, lakini utafiti mpya unaonyesha kuwa wapo amfibia watatu wa aina hiyo katika maeneo mbalimbali nchini China.

Wanasayansi wanasema kuwa mjusi huyo mkubwa amekuwa ni miongoni mwa wanyama wa pori wanaoogopwa zaidi, na wanasema kwamba watu wa hifadhi ya wanyama wanapaswa kufanya bidii zaidi kumuokoa au atatoweka ulimwenguni.

Profesa Samuel Turvey, mtafiti mkuu kutoka Taasisi ya Zoolojia ya jijini London, anasema kuwa kupungua kwa idadi ya wanyama hao kumekuwa kukitokea kwa kiasi cha kushangaza sana, sababu kuu ikiwa binadamu kutafuta lishe.

Wakati wa utafiti huo, imebainika kwamba wanasayansi walitumia viumbe hai ambavyo vina mwonekano sawa na mjusi mkubwa anayepatikana China, na kuangalia asili ya mnyama huyo ni wapi.

Wazo lao lilikuwa ni kuona kama mjusi huyoa ana utofauti na mjusi mkubwa aliyedaiwa kuwa mkubwa zaidi ulimwenguni mwaka 1920 ambaye amehifadhiwa Uingereza.

Walitaka kufahamu ikiwa mjusi wa zamani ana tabia sawa na mjusi wa punde.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...