Skip to main content

Kidosho azua kioja baada ya kuficha mikate hadi ikaoza

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 18 September 2019.

Demu kutoka mtaa wa Chepseon, kaunti ya Kericho, alizua kioja baada ya kugunduliwa alificha mikate hadi ikaoza. Hii ilikuwa baada ya sherehe katika boma lao, ambapo kidosho aliyeolewa hivi majuzi alitekwa na tamaa ya mikate iliyokuwa imenunuliwa kwa ajili ya sherehe hiyo.

Penyenye za mtaani zinaarifu kuwa kidosho alitekwa na tamaa ya mikate na akaamua kuchukua kadhaa na kuificha ghalani. Mikate hiyo ilipatikana na kijana mmoja bomani humo ikiwa imeoza na kutoa harufu mbovu.

Demu alipofumaniwa na mahojiano alikiri kuwa aliichukua miate hiyo ambayo aliisahau kwa bahati mbaya baada ya sherehe. Alizomewa na kushauriwa aache ulafi iwapo alitaka ndoa yake idumu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →