Polo Aaibika Kufika na Windo: Mwanadada Amechukuliwa na Aibu baada ya Kujivinjari na Landilodi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 17 September 2019.

Alhamisi, mwanadada alipata aibu ya mwaka alipofika plotini na mrembo aliyemuingiza boksi na kupata kufuli ya landilodi mlangoni.

Alitajwa kuwa alijitahidi kumtongoza demu huyo kwa siku kadhaa na hatimaye akafaulu kumshawishi amtembelee kwake.

Alipofika plotini, alirauka mapema kwenda stejini kusubiri windo lake, na baada ya mwanadada kuwasili alasiri waliandamana pamoja hadi plotini kujivinjari.

Walipowasili, kalameni alipandwa na mori kupata landilodi alikuwa ametia kufuli kwenye mlango wake kwa kutolipa kodi ya nyumba.

Alitajwa kuwa alianza kumlilia landilodi amfungulie chumba akiahidi kulipa baada ya siku mbili, lakini demu alikunja uso kwa dharau akifuatilia kisa hicho hadi pale ambapo landilodi alilegeza kamba na kuwafungulia mlango.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...