Skip to main content

Mbunge wa Makadara George Aladwa Amtetea Katibu wa Usalama wa Ndani Karanja Kibicho

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 16 September 2019.

Published on September 16, 2019, Mbunge wa Makadara George Aladwa amemtetea katibu wa Usalama wa Ndani Karanja Kibicho kuhusu madai kuwa anatumiwa kummaliza kisiasa Naibu Rais William Ruto.

Aladwa aliwataka viongozi wa Tangatanga kusita kumuingilia Karanja Kibicho, kwa sababu wana njama ya mambo fiche ambayo wanataka kutekeleza.

Aladwa alisema, "Nataka kumtetea Dr Kibicho na kuwaambia viongozi wawache kuhujumu kazi ya afiwa wa umma wakati ambapo anafanya kazi yake. Katibu huyo aliteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta na anaifanya kazi ya rais," alisema Aladwa.

Aladwa alisema pia kwamba viongozi hao wamezoea siasa mbaya ya matusi, ukabila na kuwatenganisha watu hali ambayo BBI itashughulikia.

Aladwa alisema, "Viongozi hao wamezoea siasa mbaya ya matusi, ukabila na kuwatenganisha watu hali ambayo BBI itashughulikia, ndi kwa sababu hawajafurahia kwa sababu nchi inazidi kuungana," alisema Aladwa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →