This archive report was first published on 15 September 2019.
Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria alikuwa katika kipindi cha kujivinjari na viongozi wengine wakiwemo seneta wa Nairobi Johnson Sakaja na aliyekuwa mwenyekiti wa Jubilee David Murathe. Picha zao zilichapishwa huku zikizua hisia kali haswa baada ya kiatu cha binti kuonekana ndani ya chumba.
Wanamtandao waliteta viongozi wanajipa raha huku Wakenya wakiteseka. Kuria alikuwa pamoja na viongozi wengine wakiwemo seneta wa Nairobi Johnson Sakaja na aliyekuwa mwenyekiti wa Jubilee David Murathe.
Wanamtandao walichukua muda na kumlima Kuria [amoja na kikosi chake wakidao kuwa wanajivinjar wakati ambapo wananchi mashinani wanateseka. Hata hivyo, Kuria hakubabaika ila aliwatolea wafuasi wake picha nyingine huku akiwa ameshikilia kinywaji cha bei ghali aina ya Hennessy.
Wanamtandao walifanya upekuzi wao kiwango cha kujaribu kumfichua mmiliki wa kiatu hicho. Picha hii ya Moses Kuria iliibuka kwenye mtandao saa chache baada ya kuonekana kwenye nyingine wakiwa na vinywaji. Picha: Okor Ya'tan