This archive report was first published on 14 September 2019.
Rais Uhuru Kenyatta aliamuru bendera ya Kenya nchini humu kupeperushwa nusu mlingoti kutoa heshima kwa Robert Mugabe, mwanzilishi wa taifa la Zimbabwe, ambaye alifariki akiwa na miaka 95, Ijumaa, Septemba 6, 2019, akiwa Singapore.
Uhuru atashiriki katika ibada ya mwisho ya Mugabe, ambayo imeandaliwa katika uwanja wa michezo jijini Harare, pamoja na viongozi wengine wa Afrika, kama vile Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Filipe Nyusi wa Mozambique, Edgar Lungu wa Zambia, Hage Geingob wa Namibia, na Teodoro Obiang Nguema wa Equatorial Guinea.
Uhuru alimuomboleza Mugabe na kumtaja kama mtu aliyejitolea kupigania uhuru wa nchi yake na kuwa mstari wa mbele kwa hali na mali kutetea masuala yanayohusu bara nzima la Afrika.
Alisema, "Ninamuomboleza Mugabe kwa kazi yake ya kujitolea kupigania uhuru wa Zimbabwe na kuwa mstari wa mbele kwa hali na mali kutetea masuala yanayohusu bara nzima la Afrika."