This archive report was first published on 14 September 2019.
Harusi ya kushangaza ilifanyika mnamo Septemba 7, 2019, katika eneo la Rimrose Valley Park, Merseyside, Uingereza.
Mwanamke wa miaka 34, ambaye pia ni mama wa watoto wawili, alifunga ndoa na mti huku ndugu, jamaa na marafiki wakijitokeza kusherehreka hafla hiyo.
Alivalia rinda la kijani wakati wa harusi hiyo, na picha zilizosambazwa mitandaoni zimefichua umbali ambao mwanadamu ananaweza kufika kulinda uhai wa miti.
Alibadilisha jina lake baada ya kupata 'mume' na kujiita Kate Rose Elder, na mchumba wake alimsaidia katika mipango ya kuandaa harusi hiyo.
Wakazi wa eneo hilo walikuwa wakilalamikia mipango ya ujenzi wa barabara ianyopaswa kupitia katikati mwa bustani hiyo, na wanaamini hatua ya Cunningham itasitisha shughuli hiyo.